Kocha wa Simba Sc, Fadlu Davids amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Mei wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2024/25 akiwashinda Miloud Hamdi wa Yanga na Rachid Touassi wa Azam alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Fadlu aliiongoza Simba Sc kushinda michezo yote mitano iliyocheza mwezi huo na kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Simba ilizifunga Singida Black Stars (1-0), KMC (1-2), Pamba Jiji (5-1), Mashujaa (2-1) na JKT Tanzania (0-1).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *