Sugu ChademaSugu Chadema

Hatimaye Sugu Atoa Msimamo Wake “Nipo Sana Chadema”

Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amebainisha kwamba bado yupo Chadema na si kweli kwamba wote waliokihama Chama hicho siku za karibuni walikuwa wakimuunga Mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Sugu amebainisha hayo leo Ijumaa Mei 23, 2025,kando ya Kikao cha kawaida cha Kamati kuu cha Chadema, Kinachoketi kwa siku mbili Jijini Dar Es Salaam, akieleza kwamba ataendelea kupambana ndani ya Chadema kwani ndilo tumaini pekee la Watanzania lililosalia.

“Hivi vitu vipo lakini vinashughulikiwaje na Chama ndiyo maana tupo Kamati kuu sasa hivi kwenda kuangalia tunaenda wapi mbele na chama chetu tukiweka mbele maslahi ya Watanzania kwasababu Chadema ndiyo tumaini pekee lililobaki la Watanzania labda pamoja na Jeshi.” Ameeleza Sugu.

Amezungumzia pia kuondoka kwa wanachama wa Chama hicho kwa siku za karibuni akieleza kwamba ni jambo la kawaida kwa Vyama vya siasa na taasisi hasa pale uchaguzi unapofanyika kutokana na baadhi yao kutoridhika na mchakato wa uchaguzi, akisisitiza umuhimu wa kutanguliza mbele maslahi ya Chama hicho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *