Kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) na Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Julius Malema, amesema kundi la Wazee (akimlenga Rais Trump na Ramaphosa) wamekutana Washington nchini Marekani kupiga umbea kuhusu yeye akisema hakuna ushahidi wa uhakika ambao Trump ameutoa kuthibitisha ubaguzi wa Wazungu nchini Afrika Kusini.

Malema amesema hawawezi kukubali kuona ardhi ya Afrika Kusini ikiporwa na Wazungu bila malipo wala fidia yoyote kwa faida za kisiasa zinazowanufaisha wachache.

Itakumbukwa jana Rais wa Marekani, Donald Trump, alimuuliza Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa walipokutana Ikulu ya White House Marekani kwamba kama Serikali yake haiungi mkono ubaguzi na mauaji ya Wazungu nchini Afrika Kusini kwanini hadi leo hawajamkamata Kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) na Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Julius Malema ambaye alitangaza hadharani mbele ya umati wa Watu kuwa Wazungu wanapaswa kuuawa na kupokonywa ardhi zao.

Trump aliuliza swali hilo muda mfupi baada ya Trump kuagiza TV iwashwe na akamuonesha Ramaphosa jinsi baadhi ya Viongozi na Wanaharakati nchini mwake akiwemo Malema walivyotangaza hadharani kile Trump alichokiita ubaguzi wa Wazungu na kuwapokonya ardhi zao, ambapo licha ya kutazama video hiyo Ramaphosa aliendelea kusisitiza kwamba Serikali yake haiungi mkono mauaji ya Watu.

Trump amehoji “Kwanini hamjakamata yule Mwanaume (Malema), amesema ‘Wazungu wauawe, waueni Wazungu’ kisha anacheza huku anarudia kauli yake, sina uhakika lakini nadhani Mtu akisema waueni Watu fulani, anapaswa kukamatwa haraka, yule alikuwa anaongea kwenye uwanja wenye mamia ya Watu na kuna Wazungu wenye mashamba yao tumeona video wameuawa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *