Mo Dewji Apewe Maua Yake, Huyu Ndio Game Changer wa Soka la Bongo
Hizi vurugu zote unazoziona kwenye Soka letu kwasasa ni baada ya Kutolewa TONGOTONGO na Bilionea MOHAMED DEWJI
Moodewji alipoamua kuwekeza Simba watu walimbeza ohhh , bahili hatafika popote, Bilionea akakaa zake kimya akaweka Mipango sawa, akafanya sajili bora na kuanza kuwapiga za kichwa
Misimu Minne Mfululizo chini ya Utawala wa MOODEWJI hakuna Timu iliyofurukuta walisotea gomba,
Uwekezaji wake ukaanza Kulipa akabena Mataji 4 Mfululizo, akaenda robo fainali ya CAF back to back , akaona haitoshi akasema atajenga Viwanja vya Mazoezi akajenga Kule Bunju
Moja ya Kauli yake aliyopenda kuirudia katika Mazungumzo yake ni ile ya “Shabaha yangu ni kuona Simba wanafika Fainali ya CAF na kubeba Ubingwa ” hakika ndoto yake inakwenda Kutimia
Nyie endeleeni Kupiga bla blaa MOODEWJI anajenga Timu tishio kwaajili ya Kupambania Mataji ya CAF ninyi mtabaki kupiga Propaganda zisizo za Msingi