Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Viongozi wapya katika taasisi mbili muhimu za umma, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya kiuongozi yanayolenga kuimarisha utendaji wa taasisi za Serikali.
Katika uteuzi huo, Abdul-Razak Badru ameteuliwa kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) ambapo Kabla ya uteuzi huo Badru alikuwa akihudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na teuzi wake unakuja baada ya nafasi hiyo kushikiliwa na Dkt. Elirehema Joshua Doriye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakati huo huo, Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho ameteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kabla ya uteuzi huu Nyansaho alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara katika Benki ya Azania.
#MillardAyoUPDATES