Afisa habri wa klabu ya Simba Sc Ahmed Ally amefunguka mambo mazito kuhusiana na watani wao wa jadi Yanga Sc mara baada ya mnyama kupoteza ubingwa wa kombe la shirikisho barani Afrika mbele ya RS Berkane kwenye mchezo ambao umepigwa siku ya jana.

Simba Sc walikuwa wenyeji kwenye mchezo huo ambao ulipigwa siku ya jana jumapili tarehe 25 Mei, katika dimba la New Amaan Complex kisiwani Zanzibar. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana 1_1.

Simba Sc wamepoteza kombe kwa matokeo ya jumla ya 3_1 kwani kwenye mchezo wa awali ambao ulipigwa nchini Morocco, RS Berkane waliwafunga Simba Sc magoli mawili kwa sifuri.

Mara baada ya Simba Sc kupoteza ubingwa huo, Ahmed Ally amewataka mashabiki, wapenzi na wadau wa klabu ya Simba Sc wasiumie mioyo yao kwani timu yao ilipambana mpaka hatua za mwisho katika kuhakikisha kwamba timu yao inabeba kombe lakini mambo yalikuwa magumu na ndio maana wamepoteza ubingwa.

Sambamba na hilo Ahmed Ally amewataka mashabiki hao kuacha kuogopa kuchekwa na Yanga Sc kwa sababu Yanga Sc wao waliishia kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kitu ambacho kinaonyesha wazi kwamba timu yao ni mbovu sana.

Ahmed Ally katika taarifa yake ameendelea kueleza kwamba mashabiki wa Yanga Sc kwa sasa wanapaswa kufananishwa na watu wajinga ambao huwa wanafurahia kifo cha wengi na wanasahau kwamba maumivu ya kufiwa hayana kujifariji kwa namna ya kwamba kifo cha wengi ni sherehe.

Taarifa hii ya Ahmed Ally imelenga kuwapooza mashabiki wa klabu ya Simba Sc ambao wameumizwa sana na matokeo ya mchezo huo ambayo yamewanyima ubingwa na hii inatokana na sababu kwamba mashabiki hawa walikuwa wanaamini kwamba huu ndio wakati wao sahihi wa kushinda ubingwa wa Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *