Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes atapewa muda hadi wiki ijayo kuamua kama anataka kuondoka katika klabu hiyo, huku Al Hilal wakipanga kutoa takriban £100m kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno, 30, ambaye angelipwa takriban £65m kwa msimu nchini Saudi Arabia. (Mirror)
Bayern Munich wanaweza kuanzisha mpango wa kumnunua Fernandes ingawa ada ya uhamisho ambayo United ingetaka inaweza kuwa kikwazo. (Teamtalk)
Winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, ana uwezekano mkubwa wa kuondoka Manchester United msimu huu wa kiangazi baada ya kukatishwa tamaa na majukumu yake chini ya kocha mkuu Ruben Amorim. (ESPN)
Wawakilishi wa Garnacho wanatazamiwa kufanya mazungumzo na Manchester United kujadili mustakabali wa Muargentina huyo baada ya kuenguliwa kwenye fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Tottenham . (Telegraph – subscription required)
Manchester United pia wanatazamia kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20, ili kupunguza shinikizo la kifedha kwa klabu hiyo.
BBC