WAKATI joto la pambano la Dabi ya Kariakoo likiendelea kupanda kwa mashabiki wa soka nchini, Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi amevunja ukimya na kuweka bayana kwamba kwa sasa anaendelea kuwaandaa wachezaji kwa mechi tatu zilizosalia kufunga msimu kwa timu hiyo, lakini dabi haipo.
Kwa mujibu wa Hamdi, Yanga inaendelea kujifua kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania Prisons ugenini Juni 18 na kumalizia nyumbani na Dodoma Jiji Juni 22 kisha fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Singida BS huku mechi dhidi ya Simba ikiondolewa kwenye ratiba ya Yanga.
“Tuna kazi kubwa ya kufanya katika mechi mbili za ligi ambazo zimebaki. Tunaamini zitakuwa ngumu kutokana na timu ambazo tunakutana nazo kuhitaji ushindi pia hasa wenyeji wetu kwenye mchezo wa kwanza ugenini haipo kwenye nafasi nzuri inahitaji pointi tatu ili kujiweka katika mazingira ya kucheza na sisi tunazihitaji ili tutetee taji,” alisema Hamdi.
.
“Kikubwa kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati, ninaamini kwamba tutafanya vizuri na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zijazo kikubwa kinachonipa matumaini ni kurejea kwa wachezaji wangu ambao hata hivyo tayari wamerudi kwenye ushindani.”
.
“Kurejea kwa Pacome na Aucho kumeongeza nguvu ukizingatia kuna mchezaji mmoja muhimu pia ameondoka kikosini Stephane Aziz Ki.” Hamdi alisema ukiondoa mechi mbili za ligi pia ile ya fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida Black Stars ambayo utachezwa kati ya Juni 26 hadi 28 wanaitaka.
.
“Sio mechi mbili tuna fainali moja pia ni muhimu kwetu tunahitaji mataji yote, hivyo kazi kubwa ni kwangu kuandaa mikakati sahihi na wachezaji kumaliza kwa kutumika vizuri dakika zote za mchezo na kuipa matokeo mazuri timu.”
ALSO READ | Yanga Wasipocheza, Simba Bingwa 2024/25